Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donuld Trump ametoa msimamo mkali wa sera yake ya kupinga uhamiaji na kutoa onyo hapo baada ya kufanya ziara nchini Mexico akisema watu wanaovuka na kuingia Marekani kwa njia haramu hawatofanikiwa hata siku moja kupewa hadhi ya ukazi halali nchini humo. Kauli hiyo ya Trump ni moja ya msururu wa misimamo yake kuhusu mpango wake wa kudhibiti uhamiaji haramu aliyowahi kuitoa mapema hapo jana wakati alipokutana uso kwa macho na rais wa Mexiko Enrique Pena Nieto. Akizungumza huko Phoenix Marekani Trump alisisitiza kwamba pindi akichaguliwa kuwa rais wa Marekani atajenga Ukuta kuzuia wahamiaji kuingia kutoka Mexico.
Suala la Uhamiaji ni suala kuu la Trump katika mapambano yake dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuelekea uchaguzi wa rais wa Novemba 8 nchini Marekani.
Mwisho wa habari/ 291